Katika mkusanyiko uitwao Sauti ya Mbinguni, tumehifadhi nyakati za hisia, ikhlasi, na uzuri wa sauti za wasomaji mashuhuri wa Qur'an kutoka Iran. Hapa tunayo klipu ya Muhammad Abbasi, qari wa kimataifa wa Iran, akisoma sehemu ya aya ya 6 ya Surah al-Ahzab. Kisomo hiki ni mfano wa uzuri wa sauti na ufasaha wa Qur'an, na kinatarajiwa kuwa daraja la kuleta ukaribu zaidi na maneno ya Wahyi.